• Please if you have anything to share with us dont fall back, upload your resources, Questions and solutions for others to benefit too.

Unawezaje pata namba za simu ulizopoteza na hujasevu kwenye email?

  • Thread starter Thread starter chrismory
  • Start date Start date
  • Replies: Replies Replies 0
  • Views: Views Views 15

chrismory

Administrator
Staff member
Joined
Oct 9, 2025
Messages
38
Watu wengi waliwahi kuruhusu Instagram isync contacts zao bila kujua. Baada ya muda, wanataka kujua: namba hizo ziko wapi? Na naweza kuzipata tena?
Hapa kuna ukweli muhimu kabla ya kuanza:
Instagram hairuhusu kuona namba za simu za watu wengine kwa siri. Kinachowezekana ni kuona data yako mwenyewe uliyowahi kuipa Instagram.
Screenshot 2026-01-20 224307.png
Hebu tuvunje vizuri.

1. Kupakua Data zako Kutoka Instagram (Njia Rasmi)​

Instagram inakuruhusu kupakua kila kitu ulichowahi kushare nao, ikiwemo contacts kama ulizisync.

Hatua:
  1. Fungua Instagram
  2. Nenda Profile → Settings & privacy
  3. Chagua Accounts Center
  4. Bonyeza Your information and permissions
  5. Chagua Download your information
  6. Chagua data unayotaka (hakikisha Contacts imechaguliwa)
  7. Subiri email ya download link (huweza kuchukua masaa au siku)

Ukishadownload, fungua folder la Contacts au Connections. Hapo ndipo utaona namba ulizowahi kusync.

au ukiona njia ya ku download file ni ngumu basi ukishafika step ya 4 utaona sehemu imeandikwa manage contacts, au click link hii kuona direct link
Hapo utaona namba zako zote ulizowahi kuwa nazo kwenye simu yako.
 
Back
Top Bottom